Mpendwa Rafiki, Namshukuru mola kwa kuweza kunijalia Afya njema, nimatumaini yakungu kuwa nawewe ni mzima wa Afya. Ni weekend safi kabisa, siku ya jumamosi ya tarehe 17 kwenye mwezi huu wa 5. Kama kawaida tunaendelea na simulizi ya Tamthilia yetu nzuri kabisa, Tamthilia ya The Second Door, na leo nawaletea Episode namba 3 ya simulizi hii.
Katika Episode ya 2 tuliweza kushuhudia jinsi ambavyo jitihada za Frank kujaribu kukata rufaa kwenye kesi ya Tarick zikigongeshwa mwamba na mtu ambae frank hakuweza kumjua ni nani, japokuwa alishahisi kuwa kunauwezekano mkubwa kwamba kunamtu ambae alikwamisha mpango huo kwa makusudi. Tukio hili zima bado linakuwa kizungumkuti kwa Frank, kwani mtu ambae angemwambia pa kuanzia alikua ni Brenda ambae mpaka hivi sasa hatma ya uhai wake ipo mikononi kwa mwenyezi mungu.
Frank anaondoka katika mazingira ya pale mahakamani na anaamua kuelekea Gerezani ambako Tarick Amefungwa, Kumbe ndani ya muda huo bila ya kufanya makosa Profesa Rweyemamu tayari alikuwa ameshafanya mpango, ikapelekwa list maalumu ya baadhi ya wafungwa ambao wamefungiwa ruhusa ya kutembelewa na mtu yoyote zaidi ya maafisa usalama. Bila kujua hilo,Safari ya Frank Inampeleka mpaka gerezani, Baada ya kufatilia Taratibu za kumuona mtu wake, maafisa waliokuwa zamu muda huo wanatizama Details za mfungwa husika, kisha wanampa taarifa frank kuwa kwa bahati mbaya mfungwa huyo yupo kwenye list ya wafungwa maalum ambao hawaruhusiwi kuonana na mtu yoyote, mpaka uandike barua ya maombi kwa Jenerali Devid Mwamkonge, halafu uandike barua nyingine ya utambulisho ipelekwe kwa mh profesa Rweyemamu. Kusikia jina la Rweyemamu, Frank anatoa tabasamu lake ambalo linataka kuwa kama tabasamu la dharau, lakini ndio maumbile yake yalivyo. Anatabasamu kwa kupinda mdomo pembeni hivi kisha anawaaga wale maofisa na kuondoka akiwaacha wameduwaa.
Kinachowashangaza zaidi maofisa hao kwanza kuona jinsi mtu ambae ndugu yake yupo kifungoni, akiwa hana taharuki ya kutaka kumuona, hasa baada ya kuzuiliwa kufanya hivyo. Rweyemamu akiwa ofisini kwake majira ja mchana, unakaribia kabisa muda wa chakula cha mchana. Yupo kwenye kikao kifupi na baadhi ya watu wake. Kikao hiki kilikuwa kikihusiana na mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa mwili wa Brenda unapatikana kwa njia yoyote ile, kumbuka wao waliamini kuwa Brenda alikuwa ameshapoteza maisha, hivyo kati ya maadhimio ya kikao hicho kifupi ilikua ni kuupata mwili wa Brenda, pili kumpata mtu alieuiba dakika chache baada ya tukio, pamoja na kumfungulia mashtaka mtu huyo.
Wanamaliza kikao na kila mtu anatawanyika. Inapita kama dakika moja hivi huku Profesa Rweyemamu, akiwa anawekaweka sawa madocument yake, mara anaingia mgeni ghafla, Rweyemamu anainua macho ghafla, na kugongana uso kwa uso na mgeni huyo, Kwa mstuko Rweyemamu anasema, ”Samba!?” mgeni huyo ambae alikua ni Frank anamjibu, “Suppries……!” Rweyemamu anaendelea kwa kusema, “Umefikaje Ofisini kwangu bila Taarifa!?” Frank huku akiongea Taratibu na kwa uhuru anajibu, “Sikufikiria kufanya hivyo, au unahisi ingesaidia kunizuia kufika hapa?” Frank anatikisa kichwa kuonesha kukataa kisha anaendelea, “ilikua lazima nionane na wewe by anyhow”, Frank akiwa anazungumza maneno hayo, Rweyemamu ana sogeza mkono wake taratibu kwenye button ya alam huku akiuliza, “Ok unataka nikusaidie nini?” Frank anamtizama kwa dharau kisha anamjibu, “Kitu cha kwanza, simamisha zoezi lako la kuita Walinzi”. Baada ya kuambiwa hivyo Rweyemamu anato mkono wake Taratibu karibu na batan Ya Alam, Frank anaendelea kwa kusema, “Halafu nisikilize kwa makini”.
Muda wote huo Rweyemamu alikua amekaa chini, Sasa Frank nae anakaa chini taratibu huku akisema. “Ni zaidi ya miaka 20 imepita, tangu mzee Edward Rosta Rweyemamu baba yako alipo muua mama yangu ili apite kwenye uchaguzi.” Baada ya sentensi hiyo frank ananyamaza kidogo Bila kuonekana na Rweyemamu anabandika kifaa kidogo kama kifungo cha koti amabacho kitaalamu kinaitwa DMR(Dynamic Micro Recording), kisha anamkazia macho Rweyemamu na kuongea kwa sauti ya chini na msisitizo,”Unakumbuka kuwa mimi na dada yangu tulibaki yatima………… tukavunjiwa nyumba yetu ya urithi, ili kupisha ujenzi wa bomba la maji……….” Mpenzi msomaji sijui nitumie maneno gani kukueleza hali aliyokuwanayo profesa Rweyemamu kipindi Frank anamwambiaa maneno hayo, lakini kwa kifupi alilowa mpakaaaaaa ……….,. Frank anaendelea, “na Fidia Mpaka leo Hatujalipwa…………. Najua hujui nini kiliedelea………, Kale kadada kangu kiliko kadogo kipindikile kalishatangulia mbele za haki, kabla ya mimi kuacha shule na kuwa mtoto wa mitaani ” Frank anakaa kimya kidogo na kuendelea, “Sasa sijaja kulipa kisasi kwa mauaji yaliyofanywa na baba yako, wala sikuja hapa kudai fidia ya nyumba yetu mlioibomoa miaka 20 iliopita, nimekuja kukupa onyo moja tu! ……………. Ukimwaga damu ya mtu yoyote asiekuwa na hatia……… Utaioga.”
Hapa panaweza kukuchanganya na wewe msomaji wangu, lakini ishu ipo hivi…, Kama nilivyotangulia kukwambia kwenye Episode za awali kabisa. Baba yake na Profesa Rweyemamu, alikua ni mwanasiasa nguli, mzee huyo enzi zake alikabiliwa na upinzani mkubwa wa kisiasa kutoka kwa mama mmoja alie kuwa na mvuto mkubwa kwenye jamii,mama huyu ni Mrs Rwambano ambae ndie mama yake na Frank. Baada ya kuona dalili zote za kushindwa kwenye mtanange huo, Mzee huyo alitumia mbinu za kishirikina kummaliza Mrs Rwambano, mbinu hizo chafu zilisababisha mama huyo akaugua ghafla mpaka kupoteza maisha. Frank na Rwambano walisoma katika shule moja ya secondary mpaka form 2 kabla ya kifo cha mama yake na Frank, baadae Frank aliacha shule kutokana na kukosa ada. Hivyo basi, licha ya kwamba frank alikua nyuma kwa kidato kimoja bado kunamikasa mizito inayoziunganisha historia zao. Rweyemamu anafahamu vizuri sana kuwa Frank ni mtu wa aina gani, Frank pia anamfahamu Rweyemamu Barabara.
Frank Anapomaliza Tu kuongea kauli hiyo anatoweka na kumuacha Rweyemamu akiwa kwenye Dilema. Rweyemamu anatoka kwenye Reception ya ofisi yake huku akiwa ametota Jasho, anamkazia macho secretary wake, kabla hajaongea Secretary wake anamuuliza,“Profesa mbona unatoka jasho hivyo!” Baada ya swali hilo Rweyemamu anajibu haraka haraka, “Air Condition Zimezimika ofisini kwangu. Rahima! ” Rahima anaitika, ”Naam Bosi ”, kisha Rweyemamu anamuuliza, “unamfahamu mgeni alieingia ofisini kwangu muda huu?” Kwa hofu Secretary anajibu, “Hap.. Hapana yeye aliniambia kuwa an….” Rweyemamu anamkatisha Secretary wake kwa hasira, “Quit! Beba mkoba wako…, unarudi nyumbani wiki mbili. Tarehe 9 Augost unaripoti hapa ukiwa na barua yenye hayo maelezo unayotaka kuniambia, Sawa? ”, Secretary huyo anaitikia kwa unyonge, “Sawa”. Rweyemamu anamalizia kwa kusema, “Haya mpigie simu mwenzako mwambie kesho aingie kazini” Akiwa mtu alie pandwa na jazba, Rweyemamu anamtizama Yule dada kwa sekunde kadhaa kisha anasema,”Ebo!” halafu anaondoka.
Frank anarudi moja kwa moja mpaka Mafichoni alikomhifadhi Brenda, Bado hali ya Brenda ni tata. Haioneshi kuwa amekata roho, lakini duniani hayupo Akhera anatafutwa, hata mapigo yake ya moyo ni kama yamesimama kabisa. Frank akiwa anazungumza na Daktari anaamua kumpa Tsh 200,000. Dokta anakataa kuchukua pesa hiyo na kusema, “Hapana Frank mimi na wewe ni kama ndugu hauitaji kunilipa”, Frank anamtazama na kumwambia, “Roby! Siitaji undugu na wewe Katika hili, You have to take full Responsibility, Kwa kuwa Brenda Hajafa, lazima uhakikishe unatumia Taaluma yako yote mpaka apate Fahamu. Na kama atatakiwa kusafirishwa nijulishe mapema. Roby…. Lazima nikulipe! Na sikulipi kwasababu wewe ni dokta au kwasababu hapa upo kazini, ila kwasababu nalazimika kugharamia uhai wa huyu binti hata kwa gharama ya damu yangu. Do your Best Please nitakulipa Doller 80 kila siku”. Hapo Frank alikuwa akizungumzia zaidi ya laki 130,000 za kitanzania. Frank anamuaga Dr Roby na kurudi kwa mama, Mama anaonekana mwenye furaha kumuona Frank, Frank anamthibitishia mama kuwa kila kitu kinaenda vizuri hivyo asijali. Licha ya hivyo frank ana muaga mama kuwa anatakiwa aondoke hapo nyumbani ili ashughulikie jambo hili vizuri, Frank anafanikiwa kumshawishi mama na kuondoka nyumbani kuelekea hotelini.
Akiwa hotelini na mizigo michache kabisa ikiwa ni pamoja na mzigo wa muhimu zaidi kwenye maisha yake ambao ni laptop yake, Frank anaweka kambi kwenye hoteli hiyo iliyopo nje kidogo ya mji ambako isingeweza kufikika au kujulikana kwa urahisi. Usiku wa siku hiyo ya wisho wa mwezi, kama ilivyo kawaida Raisi wa jamhuri alikua akihutubia taifa kama ilivyokuwa utaratibu wake wa kila mwezi. Katika hotuba yake raisi aliomba kusogezwa mbele kwa Shuguli za mahakama na magereza kwa muda wa siku kumi ili kupisha ugeni mzito ambao ulitarajiwa kufika nchini kutokea Ujerumani. Ombi hilo la Raisi Linasogeza Mbele Hukumu ya Tarick na kumpa Frank nafasi ya kujipanga vizuri zaidi jinsi ya kujaribu kumsaidia rafiki yake.
Kitendo cha kuja kwenye hoteli hii, inakua kama kambi rasmi ya Frank kuonesha kile alichokiita Upande wa pili wa sarafu. Na bila shaka kinasa sauti au DMR Device kama kinavyojulikana kitaalamu alichokuwa amebandika chini ya meza ya Prof Rweyemamu, ni kati ya nyenzo muhimu ambazo Frank anatarajia kuzitumia ili kufanikisha kazi yake.
Kesho yake asubuhi Rweyemamu huku akiongea kwenye simu anapanga kukutana na Mzee mmoja aliyekuwa mashuhuri sana kwenye ukanda wa pwani, mzee ambae inaaminika kuwa amepewa kipaji cha kuwa na maono juu ya maisha ya watu. Kunabaadhi ya watu walimwamini sana mzee huyu, lakini wengine wamuona kuwa alikua mshirikina kama washirikina wengine tu. Rweyemamu akiwa anaongea na timu yake Alfajiri hiyo anapokea taarifa maendeleo ya kutafutwa Brenda. mmoja anasikika akisema, “Tumefikia paziri mheshimiwa, kwani aliemchukua na kuondoka nae tunakaribia kumfahamu, ni mwanamke ambae alikua amevaa dila,ndie alie mbeba mgongoni na kutoka nae ”. baada ya kupokea Taarifa zote kikosi hicho kinondoka kuendelea na upelelezi wake, na rweyemamu anamuwahi Mtabibu Ustadh Kweme.
Rweyemamu anafika kwa ustadh kweme kisha ustaadh kweme anaanza kusoma Destiny ya Profesa Rweyemamu kwa ustadi mkubwa. Ustadh anaanza kwa kusema, ” Naona vitu vingi sana kwenye maisha yako, nakuona ni mtu mwenye bahati, mwenye maisha mazuri na merefu” kama unavyojua ndugu msomaji Japokuwa Rweyemamu alizaliwa, akasoma na kukulia mjini lakini Bado haiondoi asili yake kwa baba na mama yeye ni mtu wa bukoba, hivyo maneno hayo yanamfurahisha Rweyemamu na kumfanya atoe tabasamu jepesi huku akisema, “Najua, hii ni nyota ya ukoo, Baba alikua kiongozi, Babu alikua chifu, hata mama alikua kiongozi, kwahiyo tuna nyota za maisha mazuri na bahati”, Baada yamajivuno hayo ya rweyemamu kimya kifupi kinatanda. Kisha Ustadh Kweme Anaendelea, “Rweyemam! Katika maisha yako unaongozana na mtu………” Kauli hiyo ina mstua Rweyemamu, na kumfanya aongeze umakini wa kumsikuliza Ustadh. Ustadh anaendelea,”Wewe una uwezo na mamlaka, lakini mwenzio hana uwezo wala mamlaka, wewe una nguvu, lakini mwenzio ni dhaifu, wewe unamtaji lakini mwenzio dhofulihali ” usatadh ananyamaza kwa dakika nzima na kumuacha Rweyemamu akiwa ameduwaa. Ustadh Anaendelea, “Kati yenu mmoja atakuwa nuru na mwengine kivuli cha mwenziwe” Rweyemamu anadakia na kusema, “Bila shaka mimi nitakuwa Nuru, Since…… I get Everything………”anamaliza kusema maneno hayo tu Ustadh anamjibu, “Hapana! Wewe ndio utakua kivuli cha mwenzio, Na usalama wako wewe ni kutojaribu kushindana na Nuru La sivyo utazima kama jinsi ambavyo vivuli vingine hupotea, uhai wa kivuli ni nuru, nuru inapo angaza vyema ndipo kivuli chako kitanawiri, nuru ikififia ndio mwisho wa kivuli chako” Maneno hayo yanamfanya Rweyemamu apigwe na butwaa, akiwa katika hali isyokuwa ya kawaida anauliza, “Ustadh nani huyo atakae kuwa nuru! ” Ustadh anatabasamu na kusema, “Sisi tunaona mpaka pale allah anapotuwezesha, na zaidi ya hapo ni uweza wake”.
Mpenzi msomaji ama kwa hakika Safari hii haikuwa nzuri kwa Rweyemamu, Mtaalamu anampa maono magumu kabisa juu ya maisha yake. Tayari ameshamwambia kulingana na alivyooneshwa, aamini au asiamini hayo ni juu yake. Ok mimi naomba niishie hapa, mpaka katika Episode Namba 4, Usikose kuungana na mimi katika Simulizi hii ya The Secod Door.




